Saturday, 15 July 2017

ANGALIA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2017 KWA URAHISI

 ya kidato cha sita yametoka 2017. angalia hapa kwa urahisi zaidi kuwahi kutokea.                      
      unatatikiw kungiza namba za shule uliomaliza hapo. unatakiwa ucopy alaf unaedit sehemu ya namba ya shule hapo
    
          kwa mfano http://www.necta.go.tz/matokeo/ACSEE2017/results/s0227.htm




    ASANTE KWA KUCHAGUA BLOG YETU.

      


  

Saturday, 4 February 2017

MANENO YA TUNDAMAN BAADA YA KUTAJWA KWENYE LIST YA MAKONDA....

Msanii mkongwe wa bongo fleva Khalid Ramandani a.k.a Tundaman mwenye makazi yake jijini dar es salaam ambapo tar 3 february 2017 mkuu wa mkoa wa dar es salaam mh. Paul Makonda akizungumza akiwa makao makuu ya polisi kituo cha kati alisema miongoni mwa watu wanaotakiwa kufika kituoni hapo ni pamoja na Tunda......Kwa sababu mkuu wa mkoa hakutumia majina halisi kwa baadhi ya watu aliowataja tundaman anasema watu wengi walianza kumpigia simu akiwemo soudy brown na baada ya simu kuwa nyingi tundaman akaamua kufunguka na kusema kuwa sio yeye aliyetajwa na Paul Makonda bali ni mrembo na video queen ajulikanaye kwa jina la Tunda......

                   
                                                                             video queen Tunda......


Tuesday, 31 January 2017

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YAMETOKA..HAYA HAPA

Ingia hyo link kungalia matokeo ya form four na QT👇


      

Monday, 30 January 2017

ALI KIBA ANAPASWA KUSIKILIZA MASHABIKI ZAKE

Written by John jbp

 Ali Saleh Kiba al maarufu kama Alikiba ni miongoni mwa wasanii wakongwe na wakubwa Tanzania, Afrika Mashariki na pengine Afrika kwa ujumla. Ni mshindi wa tuzo zaidi ya 14 kwa mwaka 2016 ikiwezo tunzo kubwa kabisa za MTV EMA kwa kipengele cha Best African Act.


Kwa mafanikio makubwa aliyoyapata mwaka jana ikiwemo kupata mkataba mnono wa kampuni kubwa ya muziki duniani yaani Sony Music na kushinda tuzo zote hizo ndani ya mwaka 2016 ni wazi kabisa kuwa thamani ya Alikiba imepanda maradufu barani Afrika na pengine kila mfuatiliaji wa muziki Afrika angependa zaidi kumfahamu Alikiba, kufahamu kazi zake, ni wapi ametoka na wapi anakwenda.
Sekeseke lilitokea mwaka jana kwenye show ya Mombasa rocks iliyofanyika mjini Mombasa, Kenya kati ya Wizkid na Alikiba ni moja kati ya mambo ambayo yalifanya jina la Alikiba lizungumzwe sana barani Afrika haswa Tanzania, Kenya na Nigeria ambapo mitandao mbalimbali ya Nigeria iliripoti kua Alikiba anatrend sana nchini Nigeria.

Ushindi wa MTV EMA pia ambao awali alipewa Wizkid kabla haujatenguliwa na kupewa Alikiba ni mambo yaliyofanya apate attention zaidi kwenye soko la muziki barani Afrika.

Kutrend ni kitu muhimu sana katika soko la muziki kwa sasa, wasanii wengi duniani kote hata mpaka Marekani wamekuwa wakitengeneza kiki kabla ya kuachia kazi zao mpya ili kupata attention. Nafahamu kuwa msanii Alikiba amekuwa sio muumini mzuri sana wa kiki, lakini kiki kama hizi ambazo zinajitengeneza zenyewe ni dhambi kubwa kuacha kuzitumia kibiashara sababu kuna wanaotamani kutrend hata kwa kutembea uchi lakini hawazipati.

Mapema mwaka huu Alikiba alitangaza ratiba ya World Tour yake itakayoanzia South Africa kisha America na kumalizikia barani Ulaya. Kwa mujibu wa ratiba kutoka kwenye posters zake alizozipost Instagram Tour yake inaanza February mwaka huu. Hivyo mpaka ninaandika makala hii zimebaki siku tatu kufikia mwezi February.

Kati ya sehemu ngumu sana kupenya kimuziki barani basi ni Afrika Kusini na hii imetokana na ‘wasauzi’ kuthamini sana muziki wao na haikushangaza licha ya jina kubwa alilojijengea Diamond Platnumz kwenye kiwanda cha muziki barani Africa aliwahi kaririwa akisema amefanya collaboration na AKA ili kupenyeza muziki wake África Kusini.

Sasa wasiwasi wangu ni je? Alikiba anategemea kujaza viti kwa kuitegemea nyimbo ya Aje pekee? Target yake kwenye hii tour ni kuifanya iwe ya kidunia au analenga waTanzania pekee wanaoishi kwenye nchi husika? Aliahidi atatoa Aje remix ambayo ni nyimbo aliyoimba na msanii kutoka Nigeria MI Abaga lakini mpaka zimebaki siku tatu kabla hatujaingia mwezi anaoanza tour hakuna dalili ya hiyo nyimbo?

Binafsi nilidhani ingekuWa sahihi sana kama angeachia nyimbo ambayo amesharekodi mama mkongwe Yvonne Chakachaka kwa lengo la kuiteka zaidi South Africa kibiashara zaidi ili jina lake liwe kubwa nchini humo hata wakati wa Tour yake angetumia pia na fursa hiyo kufanya media tour kuitambulisha zaidi hiyo ngoma.

Nadhani si Mimi ila asilimia 98 ya mashabiki hawaridhishwi na namna ambayo Alikiba amekuwa slow sana na kutojua namna soko la mUziki linavyoenda na nini linataka. Ni jana kupitia mtandao wa instagram msanii wa maigizo ambaye pia ni shabiki mkubwa wa msanii Alikiba alipost kipande cha screenshot kikionesha ujumbe aliotumiwa na shabiki mwingine wa Alikiba DM kua Ali atapoteza mashabiki wake sababu hawapi raha wanayoitaka, siku zote amekuwa mtu wa kujiamini na kuwasibirisha mashabiki wake ambao ukweli bila wao asingekua hapo halipo leo.

Mwaka mpya umeanza kwa kasi kweli kila mtu yuko kasi lakini naona Alikiba bado yule yule

MESSI AMFANYIA KUFURU MAMA AKE

Written by John jbp

  
Lionel Messi ameonyesha fedha si chochote kwa mzazi, maana amenunua chupa mvili za mvinyo kila moja ikiwa na thamani ya pauni 430 (zaidi ya Sh milioni 1.3).
Maana yake kwa chula mbili ni Sh milioni 2.6 ikiwa ni kukamilisha sherehe ya miaka 57 ya mama yake mzazi airway Celia.

Mvinyo huo ghali aina ya Vega-Sicilia's Unico, ulionekana kwenye picha za mtandao wa Instagram wakati Messi akisherekea pamoja na mama yake.

Baadaye alitupia picha wakati Celia akiwa anasherekea na wajukuu zake.


Messi ni raia wa Argentina ambaye alihamia Hispania akiongozana na baba yake, wakati huo Messi akiwa na umri wa miaka 13.


Messi alitua Hispania akiwa amekwenda kutibiwa ugonjwa wa kukua huku akitakiwa kujiunga na Barcelona ambayo aliiomba imsadie gharama za matibabu.

Friday, 27 January 2017

ILI UFANIKIWE YAKUPASA KUFATA HAYA

Written by John jbp

Mafanikio ndilo jambo la msingi katika kila maisha ya binadamu. Lakini binadamu wengi tunakosa namna za kufanya ili tufanikiwe kihalali.

Unaweza ukawa upo kwenye hali ya kulalamika maisha yako ni magumu na unashangaa kwa nini hufanikiwi katika maisha yako kama jinsi unavyotaka wewe. Hali hii inaweza ikawa inakuumiza pengine kila ukiangalia rafiki zako ama maisha ya wengine yanavyozidi kuwa mazuri, wakati wewe upo katika hali ngumu. Na pengine umekuwa ukijiuliza nini siri kubwa  ya mafanikio yao ambayo wanaitumia ambayo wewe huna. Kutokana na hali hiyo umekuwa ukijilaumu kujilaumu na kujiuliza kwanini nyingi ambazo hazina majibu. Kitu usichokijua watu hawa huwa wanatumia mbinu Fulani kufanikiwa.

Kawaida, katika maisha kama ulivyomchezo wa miguu, au michezo mingine mara nyingi huwa zipo mbinu za kufanikisha kile tunachokifanya. Mbinu hizi huweza kutambulika kama sheria, kanuni, au siri lakini zote hulenga kukufanikisha kama unataka mafanikio ya kweli. Mbinu hizi zinapotumiwa kwa bahati mbaya au nzuri huwa hazifanyi ubaguzi zinamwendea yoyote na kuleta matunda unayoyataka. Hata kama ikitokea umezitumia mbinu hizi kwa bahati mbaya bila kujijua ni lazima utafanikiwa katika maisha yako.

Mbinu hizi ndizo wanazozitumia wengi wenye mafanikio na kuwafanikisha, ingawa huwa sio kwao kuwa rahisi kukwambia mbinu hizo. Haijalishi unaishi kwa sasa maisha gani au upo kwenye matatizo mengi vipi, ukizitumia mbinu hizi, zitakufanikisha na kukupa maisha ya mafanikio unayoyataka. Acha kulalamika tena na kuishi bila amani. Sasa unaweza ukawa na mafanikio makubwa kama hao unaowaona wamefanikiwa, ikiwa utatumia mbinu hizi kukufanikisha. Unajua mbinu hizi ni mbinu zipi?

Hizo Ndizo Mbinu 5 Za Kukupa Maisha Ya Mafanikio:-

1. Kuwa na nidhamu binafsi.

Ili kupata mafanikio makubwa unayoyahitaji sio suala la kufanya kazi kwa bidii tu, zaidi unachohitaji nikuwa na nidhamu binafsi ambayo itakuongoza kwenye malengo yako. Watu wengi hawana nidhamu binafsi kitu ambacho kinapelekea wengi ndoto zao zinaishia kati. Ni muhimu kuelewa kuwa ni lazima kufanya mambo yale yanayoendana na ndoto zako, hata kama kuna wakati unajihisi umechoka unalazimika kujikaza kufanya jambo hata dogo ambalo litakufikisha kwenye malengo yako. Ukishindwa kuwa na nidhamu binasi katk maisha yako elewa kuwa utashindwa kufikia mipango na malengo iliyo jiwekea.


2. Jifunze kila mara kwa watu waliofanikiwa.

Hii itakusaidia kujua vitu vingi usivovijua kuliko kukaa na kung’anga’nia mbinu zilezile ambazo hazikusaidii. Yapo mambo mengi sana usiyoyajua ambayo yanakufanya ushindwe kufanikiwa. Ikiwa utakuwa na uwezo wa kujifunza kwa wale waliofnikiwa utakuwa upo kwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa na kusonga mbele. Maisha yako yanazidi kuwa magumu siku hadi siku, kutokana na kukosa kujifunza kwa wengine kwa kujua hilo badili mwelekeo wako na kuwa mtu wa kujifinza mwisho wa siku mafanikio yatakuwa makubwa kwako.

3. Jifunze kutokana na makosa uliyofanya.

Inawezekana kuna mahali utakuwa umekosea kwa namna moja au nyingine,badala ya kulaumu na kuumia moyo sana jifunze kutokana na hayo makosa liyoafanya ili isije ikawa kwako rahisi kufanya makosa yaleyale kwa mara nyingine. Ikiwa utajifunza kutokana na makosa na kufanyia kazi kile ulichojifunza hapo utakuwa umechukua hatua moja muhimu ya kuweza kukusaidia kusonga mbele kuyafata mafanikio unayoyataka. Unataka mabadiliko makubwa katika maisha jifunze kutokana na makosa yako na acha sana kulaumu.

4. Jenga tabia ya kujisomea kila siku.

Hili ni jambo ambalo nimekuwa nikiliongelea sana kuhusu huu umuhimu wa kujisomea. Unapojisomea unapata vitu vingi sana tena ndani ya muda mfupi. Kupitia huko utaweza kujifunza mambo mazuri yatakayoweza kubadili maisha yako kwa sehemu kubwa na kuwa mtu, tofauti kabisa. Acha uvivu jifunze vitu vipya kila siku. Unaweza ukajifunza kupitia vitabu, ama mitandao mizuri inayoelimisha kama huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kupata maarifa bora na sahihi kabisa. Unapojifunza inakusaidia kukabiliana na changamoto nyingi, ambapo kwako ingekuwa ngumu kuzikabili.

5. Kuwa na mahusiano sahihi na watu waliofanikiwa.

Katika kutafuta mafanikio ni vizuri ukawa na mahusiano ama mtandao na watu sahihi ambao watakusaidia kukufikisha kwenye lengo ulilojiwekea. Haina haja kuwa na watu ambao hawakusaidii kutimiza malengo yako. Watu hawa watakukwamisha na kukurudisha nyuma katika maisha yako tu siku zote. Jenga tabia ya kuwa na watu sahihi ambao utajifunza kitu kwao, utashirikiana nao na kujifunza mambo mengi huko ya mafanikio na hatimaye utamudu kusonga mbele.

Unaweza kubadili maisha yako, kama utafanyia kazi mbinu hizi. Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, karibu katika mtandao huu wa DIRA YAMAFANIKIO uendelee kupata maarifa bora yatakayoweza kuboresha yako, kwa pamoja tunaweza.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE

HATIMAE ABAM BARROW AWASILI GAMBIA JANA.

Written by John Jbp

Rais wa Gambia awasili nchini kwake jana baada ya kukaa takribani wiki mbili senegal.
media
Rais wa Gambia Adama Barrow akiwasili katika uwanja wa ndege wa Banjul, Januari 26, 2017.
Rais mpya wa Gambia Adama Barrow amewasili mjini Banjul Alhamisi alaasiri akitokea mjini Dakar nchini Senegal ambako alikua akiishi uhamishoni tangu wiki mbili zilizopita. Umati wa watu wamekusanyika karibu na uwanja wa ndege katika mji mkuu wa Gambia kwa kumlaki.
Rais mpya wa nchi ya Gambia aliapishwa tarehe 20 Januari katika mji mkuu wa Senegal kwa sababu za kiusalama nchini mwake, baada ya rais aliyelazimishwa kuondoka nchini humo Yahya Jammeh kupinga kuachia ngazi.
Rais Adama Barrow aliomba kuendelea kwa operesheni ya kikosi cha Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) nchini mwake, iliozindua Januari 19 kwa minajili ya kumlazimisha Yahya Jammeh kuondoka madarakani, na kusem akuwa mazingira ya kiusalama hayatoshi kwa kurejea nchini.
Itakumbukwa kwamba Rais Yahya Jammeh aliondoka nchini Gambia Januari 21 jioni baada ya timu ya usuluhishi kujaribu mara kadhaa kumshawishi bila mafanikio.
Bw Barrow ameomba majeshi ya ECOWAS kusalia nchini Gambia kwa muda wa miezi sita ili kusaidia jeshi la Gambia kujipanga sawa na kurejesha hali ya utulivu baada ya miaka 22 ya utawala wa Yahya Jammeh.
Rais mteule wa Gambia Adama Barrow (katikati) akiondoka katika uwanja wa ndege wa Banjul, akizungukwa na umati wa watu.

Monday, 23 January 2017

MANENO YA TUNDU LISSU BAADA YA UKAWA KUKOSA NAFASI BAADHI YA MAENEO KATIKA UCHAGUZI WA MARUDIO.

Written by john jbp

Alichokisema Tundu Lissu Baada ya Ukawa Kushindwa Kufurukuta Katika Uchaguzi wa Marudio..!!!..Fahamu zaidi hapa.

Anaandika Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu.

Waheshimiwa na makamanda poleni kwa mapambano na hongereni kwa kazi kubwa mliyoifanya kwenye chaguzi hizi. Naona kila mmoja wetu anasikitika jinsi matokeo ambavyo yamekuwa tofauti na matarajio yetu na kazi tuliyoifanya.

Ni rahisi, katika mazingira haya ya kushindwa na kabla vumbi halijaisha, kuanza kulalamika, kunyoosheana vidole na kukatishana tamaa. Hii haitusaidii sana. Badala yake, tunachohitaji zaidi ni 'brainstorming' kuliko 'blamestorming.' Naomba nifanye ya kwanza. Chaguzi ndogo za ubunge au udiwani ni ngumu sana kushinda katika mazingira halisi ya nchi yetu.

Mifano michache inathibitisha ukweli huu. Katika election cycle ya '05-'10, tulishinda Jimbo la Tarime lakini tukapigwa Biharamulo Magharibi na Busanda. Tarime lilikuwa Jimbo letu tangu Uchaguzi Mkuu wa '05, Busanda lilikuwa la maCCM na Biharamulo Magharibi lilikuwa la TLP. Sikumbuki vizuri kama tulishinda Kata hata moja katika mzunguko wa uchaguzi wa kipindi hicho.

Katika election cycle ya '10-'15, tulipigwa Igunga licha ya kazi kubwa tuliyofanya, lakini tukashinda Arumeru Mashariki iliyokuwa chini ya maCCM. Vile vile tulishindwa Kalenga, Chalinze na Ulanga Magharibi yaliyokuwa ya maCCM tangu Uchaguzi Mkuu wa '10.

Kwenye chaguzi za Kata za '12 kama mnakumbuka, licha ya kazi kubwa na rasilimali nyingi, tulipata Kata tatu tu kati ya 26 zilizokuwa zinagombaniwa. Ukiachia Ifakara Mjini ya Mh. Juakali, Kata nyingine mbili - Kiboriloni na Iseke - zilikuwa zetu tangu Uchaguzi Mkuu wa '10.

Kwa mantiki hii, matokeo ya jana sio ya kushangaza sana. Kata ya Duru ilikuwa ya kwetu na tumeitetea, nyingine zote tulikopigwa zilikuwa za maCCM. Hatujanyang'anywa iliyokuwa yetu, hatujanyakua zilizokuwa zao. Hata hivyo, funzo kubwa zaidi la historia ya chaguzi hizi ni hili hapa: licha ya kupigwa kwenye chaguzi ndogo hizi, tumeendelea kufanya vizuri zaidi katika kila Uchaguzi Mkuu uliofuatia kipigo cha chaguzi ndogo.

Mwaka '10 tulifanya vizuri zaidi licha ya kupigwa Busanda na Biharamulo Magharibi katika mzunguko wa '05-'10. In fact, tulichukua Jimbo la Biharamulo Magharibi mwaka huo. Na tulipata Kata nyingi zaidi '10 kuliko ilivyokuwa '05. Mwaka '15 tulipata ushindi mkubwa zaidi katika Kata na majimbo licha ya kupigwa kwenye chaguzi ndogo za mzunguko wa '10-'15.

Hoja yangu hapa ni kwamba uchaguzi wa marudio hauna direct and negative bearing kwenye matokeo yetu ya Uchaguzi Mkuu unaofuatia. On the contrary, uchaguzi wa marudio unatupa fursa ya kupanda mbegu ambayo, ikitunzwa vizuri, inakuwa na mazao bora kwenye chaguzi zinazofuatia.

Kwa upande mwingine, chaguzi za marudio - kwa sababu ya udogo au uchache wa maeneo yanayogombaniwa - yanawapa maCCM fursa ya kutumia nguvu kubwa za rasilimali na za kidola ukilinganisha na tunazotumia sisi. Kwenye Uchaguzi Mkuu unaofuatia, nguvu hizo zinasambazwa nchi nzima na kwa hiyo effectiveness yake inapungua.

Ndio maana tumefanya vizuri zaidi kwenye Uchaguzi Mkuu kuliko kwenye chaguzi ndogo za marudio. Hili, kwa maoni yangu, ndilo fundisho kuu la chaguzi hizi za marudio. Hatuna sababu kubwa ya kushangilia kutokana na matokeo ya jana. Hata hivyo, hatuna sababu yoyote ya kuomboleza pia. Obviously, maCCM na wapambe wao wataandika 'wasifu wa marehemu' wa CHADEMA/UKAWA na kuutangaza dunia nzima na kwa sauti kubwa. Hilo lisitupofushe macho yetu, hata kama linakera sana.

Tutathmini kazi tuliyoifanya na matokeo tuliyoyapata. Tupate mafundisho sahihi ya kazi hiyo na matokeo yake. Tutumie mafundisho hayo kwa kujipanga vizuri zaidi kwa ajili ya 'the real prize': 2020.

ZITTO KABWE ASAKWA NA JESHI LA POLISI.

Written by john jbp

Zitto Kabwe Asakwa na Jeshi la Polisi kwa Uchochezi.....ACT Wazalendo Wadai Yuko Salama, Wataka Polisi Wafuate Utaratibu.Fahamu zaidi hapa.

Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo ndugu Msafiri A Mtemelwa ametoa taarifa kuwa kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Mh Zitto Kabwe hajakamatwa na polisi na kusema yupo salama hapa hapa nchini.

Akitumia mtandao wa twitter wa Chama cha ACT Wazalendo Msafiri Mtemelwa anadai kuwa kiongozi huyo wa chama yupo salama lakini dereva wake ndg Patrick Muhidin pamoja na katibu wa Chama wa jimbo la Kahama ndg. Vincent Ikerenge ndio walikamatwa na walipelekwa kituo cha polisi Kahama na kuandikishwa maelezo.

"Tunawajulisha kuwa kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe, Mb hajakamatwa na polisi na yupo salama hapa hapa nchini. Tarehe 21/1/2017 Polisi wilayani Kahama wakiwa na magari 7 kati yao manne ya FFU walivamia mkutano wa Kampeni wa Chama katika kata ya Isagehe, Halmashauri ya Mji wa Kahama. Kiongozi wa Chama alikuwa jukwaani wakati polisi wanafika na aliendelea na hotuba yake mpaka mwisho na kumnadi Mgombea ndg Ibrahim Masele. Baada ya kushuka jukwaani, Kama kawaida yake alipeana mikono na wananchi na baadaye alipotea katika eneo Hilo" alisema Msafiri Mtemelwa

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo ndugu Msafiri Mtemelwa anadai wamefuatilia polisi kutaka kujua kwanini kiongozi wa Chama chao anatafutwa na polisi na kusema wamejulishwa kuwa ana mashatka ya kutoa lugha ya uchochezi katika hotuba zake za kampeni.

"Tumejulishwa na polisi kwamba Kiongozi wa Chama  ana mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi katika hotuba zake za kampeni katika kata ya Isagehe Jimbo la Kahama Mjini. Polisi wanasema Zitto Kabwe amemchonganisha Rais na wananchi kwa kusema kuwa Rais anakula bure na kulala bure ndio maana hajali hali ngumu ya maisha ya wananchi wakati huu wa balaa la njaa" ameandika Mtemelwa

Hata hivyo mbunge huyo wa Kigoma mjini na kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo kupitia viongozi wa chama cha ACT Wazalendo amesema polisi wataweza kumkamata iwapo yeye atataka kukamatwa na siyo kwa kuvamiwa bali kwa kuitwa rasmi na polisi na kuelezwa makosa yake.

"Chama kinalitaka jeshi la polisi kufuata taratibu za kukamata raia kwa mujibu wa sheria na pia protokali za kuwaita polisi viongozi wa Kitaifa Kama ilivyo kwa ndg Zitto. Chama kinajiandaa na wanasheria wake ili kwenda na KC kituo chochote cha polisi nchini Mara watakapopata wito wa kwenda polisi.". Amesema Msafiri Mtemelwa

YAHYA JAMMEH AIACHA SERIKALI YA GAMBIA BILA PESA.

Written by john jbp

 YAHYA JAMMEH AONDOKA GAMBIA NA UTAJIRI MKUBWA HUKU AKIACHA SERIKALI BILA PESA

 
Yahya Jammeh aondoka Gambia, nakuacha hazina tupu
Yahya Jammeh aondoka Gambia, nakuacha hazina tupu. Mshauri maalumu wa Rais wa Gambia Adama Barrow amesema zaidi ya dola za Kimarekani milioni 11 zinaaminika kutoweka katika hazina ya serikali, kufuatia kuondoka madarakani kwa mtawala wa muda mrefu Yahya Jammeh.
Mia Ahmad Fatty amewaambia Waandishi wa habari katika mji mkuu wa Senegal Dakar kwamba wataalamu wa masuala ya fedha wanatathmini kujua ni kiasi gani kwa sasa kimepotea.
Amesema Gambia kwa sasa ina tatizo kubwa kifedha kwa hazina yake kutokuwa na kitu.
Kwa sasa Rais Barrow amekuwa akifanya kazi na timu ya wataalamu wa masuala ya fedha na wengine kutoka Benki kuu ya nchi hiyo kupata kiasi halisi kilichopo.
Habari zinasema magari ya kifahari na mali nyingine zilionekana zikipakiwa katika ndege ya mizigo ya Chad kwa niaba ya Rais Jammeh siku alipoondoka nchini humo.
Maelfu ya watu walikusanyika katika Ikulu ya nchi hiyo jana jioni wakiyaangalia majeshi ya Senegal yakiingia kwa ajili ya kuweka usalama kabla ya kurejea nchini kwa Adama Barrow.
Adama Barrow akiwa Dakar, Senegal Januari 20, 2017
Adama Barrow, (katikati), amesema anapanga kuchunguza tuhuma za ukiukaji wa haki za kibinadamu zilizotekelezwa wakati wa utawala wa Jammeh
Rais Barrow yupo nchini Senegal na bado haijulikani ni lini hasa atarudi Gambia na kuingia ofisini.
Alisema atarejea tu baada ya kuhakikishiwa usalama wake.
Wanajeshi wa Senegal wakishika doria karibu na ikulu ya rais mjini Banjul Jumapili
Wanajeshi wa Senegal wakishika doria karibu na ikulu ya rais mjini Banjul Jumapili