Hi ni fursa kwa mtanzania na asiye mtanzania kujua historia ya Tanzania kinagaubaga. Embu tuione
Hiki ni kipindi cha historia ya Tanzania ambapo unaelezwa mfululizo wa matukio makubwa yanayohusu wananchi wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na Zanzibar, na eneo la zamani la Tanganyika na maeneo yanayoizunguka Tanzania kabla ya ukoloni wa Kizungu.
Makazi ya watu katika kanda yalianza angalau miaka 100,000 iliyopita. Ushahidi wa kiakiolojia unaonesha uwepo wa sokwe watu katika kanda hii kwa zaidi ya miaka milioni 3 iliyopita na Paranthropus kwa zaidi ya miaka milioni 2 iliyopita.
Mawasiliano ya Wazungu katika Afrika ya Mashariki yalifanywa mnamo karne ya 15 na mpelelezi wa Ureno, Vasco da Gama. Aliwasili mjini Kilimane (sasa hivi Tanzania) kunako mwaka wa 1498.
Zanzibar, funguvisiwa vilivyopo majini mashariki kwa Tanzania bara, vilichukuliwa na Dola la Ureno likabaki kuwa eneo lake kwa takriban miaka 200 hivi.
Baadaye eneo lile likachukuliwa na Sultani wa Oman mnamo 1698.
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ilianzishwa Tanzania bara mnamo 1885 na Zanzibar ikawa chini ya udhibiti wa Uingereza mnamo1890.
Miaka sita baadaye, Vita ya Zanzibar na Uingereza ilipigwa kisiwani humo, moja kati ya vita vifupi mno katika historia.
Chifu Mkwawa wa kabila la Wahehe na wapiganaji wake walipinga utawala wa kikoloni katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.
Mfano wao ulifuatwa baadaye na kikosi kizima cha makabila ya kusini katika Vita ya Maji Maji.
Hekaheka za Kijerumani ziliisha baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia wakati Uingereza ulichukua Tanganyika kwa mamlaka yaShirikisho la Mataifa.
Vikundi vya kijamii na kisiasa vilianza kazi ya kuhamasisha watu katikati ya karne ya 20.
Uhuru wa Zanzibar kutoka kwa Waingereza ukapatikana mwaka uliofuata, halafu wananchi wakamfukuza sultani.
Nyerere aliongoza nchi kwa chama kimoja kwa zaidi ya miaka 20, huku akitambulisha maoni yake juu ya Usoshalisti wa Kiafrika,Ujamaa.
Aliachia ngazi mnamo 1985 akafuatiwa na Ali Hassan Mwinyi.
Benjamin Mkapa, rais wa awamu ya tatu nchini, alishinda uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi Tanzania mnamo 1995. Wakati wa urais wa Mkapa, Tanzania iligushiuhusiano wa kidiplomasia katika kanda kwa kusaini Mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Mwaka wa 2003, jenasi mpya ya ngedere imegunduliwa nchini, ya kwanza kugunduliwa tangu mwaka wa 1923.
Rais Jakaya Kikwete alichaguliwa mnamo2005 na kuongoza hadi 2015. 2015 mpaka sasa anatawala rais Magufuli wa chama cha mapinduzi.
No comments:
Post a Comment