Sunday, 27 November 2016

Hizi ni fursa kadhaa waweza kuzifanyia kazi ili uweze kufanikiwa

 Katika maisha binadamu wengi tumekuwa tukitamani kufanikiwa katika maisha,,lakini bdo wengi wetu hatujajua tunafanya nin tuweze kufanikiwa. Kuna namna nyingi saana ambazo unaweza ukatumia na kufanikiwa. Sasa zifuatazo ni fursa chache ambazo unaweza kuzitumia ukafanikiwa ila tu wapaswa kuwa na juhudi na uvumilivu.
   
Twende kwa pamoja kuzijua biashara hizo ambazo unauwezo wa kuzifanya na kukufikisha kwenye mafanikio makubwa:-

1. Kutengeneza na kuuza chaki

Hii ni moja ya biashara nzuri unayoweza kuifanya na soko lake liko juu. Unaweza ukanunua mashine yako za kutengeneza chaki na kisha ukaanza kuzisambaza kwenye stationary au mashuleni. Uzuri wake mashine hizi za kutengenezea chaki gharama yake pia sio kubwa sana ni ya kawaida tu ambayo hata wewe unaweza kuimudu. Hii inaweza ikawa ni sehemu mojawapo ya kuingizia kipato chako.

2. Kufungua duka la kuuza asali


Uzuri wa bidhaa hii muda mwingi soko lake lipo juu. Ni biashara ambayo unaweza ukaifanya kwa kuagizia asali kutoka kwa wakulima kama nilivyo mimi na kisha kuanza kuiuza moja kwa moja katika vipimo vinavyotakiwa.

Kama huwezi kufungua duka hili unaweza ukafanya mbadala wake ukaenda kutengeneza mizinga wewe mwenyewe na kuwafuga. Pia hii ni biashara ambayo ni nzuri kwako kukuingizia kipato kikubwa kwa urahisi.

3. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika matamasha mbalimbali

Hapa siyo lazima uwe na Hotel au Mgahawa ndiyo uanzishe biashara ya namna hii. Kikubwa unahakikisha unakuwa makini na sherehe katika eneo ulilopo. Kama ni kuweka mawakala watakao kusaidia kukujulisha kuwa eneo fulani kuna sherehe ya aina fulani na siku fulani itakuwa nzuri zaidi kwako kuchangamkia tenda hizo mapema.

4. Kujenga nyumba za kulala wageni

Kama mtaji wako unaruhusu hii ni moja kati ya biashara nzuri kuifanya. Ni biashara ambayo hahitaji kukimbizana sana ukishamaliza kujenga, zaidi unatakiwa kuweka mfumo sahihi wa kusimamia na kuanza kuingiza pesa. Na kwa bahati nzuri kwa Tanzania yapo maeneo mengi ambayo yanauhitaji mkubwa wa huduma hii. Ni Biashara nzuri kuifanya hata kama umri umeenda, kwa sababu haihitaji mkimbizano mkubwa.

5. Kutengeneza matoroli/mikokoteni na kuikodisha

Katika hili hapa unatakiwa kutengeneza kwa idadi unayoitaka na unamwachia kijana ambaye anaikodisha huku ukiendelea na majukumu mengine. Unaweza ukaiona ni biashara ndogo lakini fuatilia kwa waliowekeza nguvu na mawazo yao hapo wakwambie kile wanachokipata utashangaa.

6. Kuazisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZYPESA

Hakuna ubishi hii ni moja ya huduma ambayo imezagaa kila eneo na watu wengi wanaihitaji. Kikubwa ni juhudi yako na kuzingatia eneo uliloweka biashara yako liwe hasa la mzunguko mkubwa zaidi kukuwezesha kufanya biashara hii vizuri.

7. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe

Pia unaweza ukajiingiza hapa na kushughulika na kupamba tu maharusi. Kama hujui sana ni kitu cha kujifunza pia, kisha unachangamkia sherehe zinazojitokeza mjini.

8. Kuanzisha kilimo cha kisasa

Wengi wanaposikia kilimo kichwa kinakataa. Lakini ikiwa utawekeza kwenye kilimo cha kisasa na cha kitaalamu ambacho unategemea kumwagilia zaidi, uwe na uhakika unatoka. Yapo mazao mengi unaweza ukalima lakini mojawapo ni kitunguu. Inaweza ikawa ni njia rahisi ya kufikia mafanikio yako kuliko unavyofikiri.

9. Mashine za kusaga na kukoboa nafaka

Pia unaweza ukajitengenezea kipato chako na kuwa kikubwa na cha uhakika kwa kufunga mashine hizi. Kila siku watu wanahitaji kula hivyo ukifunga mashine hizi ni rahisi sana kupata wateja wa kuwauzia unga na kupata faida. Na uzuri mahindi ya kusaga yanapatikana maeneo mengi kwa wingi kama kule Kibaigwa (Dodoma), Gairo(Morogoro), Kiteto(Manyara) na maeneo mengine mengi kama Iringa na mbeya.

10. Yadi kwa ajili ya kupaki magari

Kitu unachotakiwa hapa ni kununua kiwanja na kukigeuza kuwa yadi ambapo magari yanakuwa yanapaki iwe kwa kulala au kwa muda. Kila gari linalokuwa linapaki linakuwa linatozwa kiasi fulani cha pesa ambacho kinakuwa ndiyo hiyo huduma unayoitoa.

  By John jbp 

No comments: