Waendesha mashtaka nchini spain wamemtaka mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa Brazil Neymar jr kuhudumia kifungo cha miaka 2 jela kufuatia kuhusika kwake katika kesi ya ufisadi kuhusu uhamisho wake kutoka klabu ya Santos nchini Brazil mwaka 2013 kwenda barca.
Jaji Jose Perals pia ametaka aliyekuwa rais wa Barcelona sandro Rosell kuhudumia kifungo cha miaka 5 jela mbali na kupigwa faini ya Euro milioni 7.2 kwa klabu hiyo.
Imetaka kutupiliwa mbali kwa mashtaka dhidi ya rais wa sasa wa klabu hiyo Josep Maria bartomeu.
Katika kesi hyo Rosell,Neymar na babake wanatarajwa kushtakiwa.
Kesi hiyo inatokana na malalamishi ya kundi la uwekezaji la Brazil DIS ,ambalo linamiliki asilimia 40 ya haki za uhamisho wa Neymar na linadai lilipata fedha chache ikilinganishwa na zile lililotarajia.
Rosell alijiuzulu kama rais wa klabu hiyo mwaka 2014 kwa jukumu lake katika uhamisho huo na kutoa ushahidi mahakamani mnamo mwezi Februari pamoja na Bartomeu,Neymar na babake Neymar.
No comments:
Post a Comment