kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la fredrick richard amejinyonga baada ya kusalitiwa na mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la rose. marehemu fredrick amefikia uamuzi huo baada ya mpenzi wake huyo (rose) kumsaliti na kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na rafiki wa fredrick aitwaye robert na kuwa katika mipango ya kufunga pingu za maisha (ndoa). kabla ya kutoa uhai wake fredrick aliandika waraka ambao ulisomeka hivi "mimi Fredrick Richard nimeumia sana tena sana juu ya mapenzi. niliyempenda na kumgaramia kwa kila hali kuamua kunifanya nifikie uhamuzi huu. Robert umeamua kumchukua mpenzi wangu ambaye ulijua kuwa ni shemeji yako, cheo chako kazini umeona kama fimbo ya kunichapia. Rose mpenzi wangu umeamua kwenda kwa rafiki yangu na kuniacha nakushukuru sana, nisingependa kuiona harusi hiyo wiki ijayo bora nife kuliko kusubiri kuumia na dharau hii toka kwa marafiki na wafanyakazi wenzangu, niwatakie maisha mema. MWISHO Poleni wazazi wangu, marafiki zangu na wote tulio kuwa pamoja naomba taarifa wapewe wazazi wangu na familia yangu kutoka musoma na tarime namba zao 0752431811." mwisho wa waraka huo wa kusikitisha. Ungemshauri nini fredrick kama ungepata nafasi kabla ya kifo chake.
u
u
Marehemu fredrick enzi za uhai wake
MANENO YA MWISHO YA FREDRICK KABLA YA KUJIUA
No comments:
Post a Comment