Saturday, 19 November 2016

PAPA AMETEUA MAKADINALI WAPYA 17 SEHEMU MBALIMBALI DUNIANI

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis amewateua makadinali wapya 17 wa kanisa katoliki kote duniani, huku mmoja wao akitokea bara la afrika.
     
       Makadinali hao wapya wanatoka mabara matano akiwemo mjumbe wa Vatican nchini Syria.
Sasa Papa Francis amechagua theluthi moja wa makadinali ambao watamchagua mrithi wake.
Ni makadinali walio chini ya miaka 80 tu ambao wanaweza kumchagua Papa mpya. 13 kati ya wale walioteuliwa wako chini ya miaka 80 na sasa wanahitimu kumrithi.
Pia papa amemteua askofu Dieudonne Nzapalanga kuwa kadinali wa bangui huko afrika ya kati
      

No comments: