Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, alizomewa kwenye ukumbi wa tamthilia mjini New York.
Bwana Pence alikwenda kuona tamthilia yenye maadhi ya muziki, ijulikanayo kwa jina la Hamilton, ambayo inaeleza maisha ya mmoja kati ya watu walioanzisha taifa la Marekani baada ya kupata uhuru mnamo 1776, Alexander Hamilton.
Pence alizomewa kabla na wakati tamthilia inaendelea.
Mwisho wa tamasha, mchezaji mmoja alisoma barua kwa Bwana Pence, kuonesha wasiwasi kuwa serikali mpya haitalinda na kutetea haki ya watu wa rangi nyeusi
Kwenye picha ni mike pence na rais mteule wa marekan Donald Trump
No comments:
Post a Comment