RAIS, Dr John Magufuli, amefanya uteuzi wa wenyeviti wawili wa bodi za mifuko ya kijamii PSPF na LAPF pia amamteua profesa satta kuwa mkuu wa chuo cha usimamizi wa fedha IFM.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi IKULU,Dar es salaam imewataja walioteuliwa kuwa ni mhandisi Alhaji Mussa Iyombe aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).
Mhandisi Iyombe ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Rais Magufuli pia amemteua Profesa Faustine Karani Bee kuwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF).
Profesa Karani Bee ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi.
Lakini pia Rais Magufuli amemteua Profesa Tadeo Andrew Satta kuwa Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Kabla ya uteuzi huu Profesa Satta alikuwa kaimu mkuu wa chuo cha usimamizi wa fedha(IFM).
KILA LAKHERI KATIKA UTENDAJI WENU.
No comments:
Post a Comment