Monday, 23 January 2017

RAIS WA UTURUKI AWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA WAZIRI MKUU.

Written by john jbp

RAIS WA UTURUKI AWASILI NCHINI.
 Rais wa  Uturuki,  Mheshimiwa, Recep Tayyip Erdogan akiongozana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam kwa ziara rasmi Januari 21, 2017.Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   na Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan  aliyefuatana na  mkewe, Mheshimiwa Emine Erdogan (kulia) wakifuhia ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage jijini Dar es salaam baada ya Rais huyo  kuwasili kwa ziara rasmi nchini Januari 21, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JE WAJUA..!!?? CHAKULA KIKUU CHA NYANGUMI NI DAGAA KAMBA. NYANGUMI NI MOJA YA SAMAKI WAKUBWA ZAIDI DUNIANI NA HUPENDELEA KULA DAGAA KAMBA NA KWA KAWAIDA NYANGUMI MKUBWA HULA WASTANI WA DAGAA KAMBA 4000000 (MILIONI NEE) KWA SIKU. ILI NYANGUMI ASHIBE VIZURI ANAHITAJI KILO 3600 ZA CHAKULA KWA SIKU
Image result for NYANGUMIKATI YA NYANGUMI WAKUBWA


BY;
CUCCITTINI.

Sunday, 22 January 2017



kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la fredrick richard amejinyonga baada ya kusalitiwa na mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la rose. marehemu fredrick amefikia uamuzi huo baada ya mpenzi wake huyo (rose) kumsaliti na kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na rafiki wa fredrick aitwaye robert na kuwa katika mipango ya kufunga pingu za maisha (ndoa). kabla ya kutoa uhai wake fredrick aliandika waraka ambao ulisomeka hivi "mimi Fredrick Richard nimeumia sana tena sana juu ya mapenzi. niliyempenda na kumgaramia kwa kila hali kuamua kunifanya nifikie uhamuzi huu. Robert umeamua kumchukua mpenzi wangu ambaye ulijua kuwa ni shemeji yako, cheo chako kazini umeona kama fimbo ya kunichapia. Rose mpenzi wangu umeamua kwenda kwa rafiki yangu na kuniacha nakushukuru sana, nisingependa kuiona harusi hiyo wiki ijayo bora nife kuliko kusubiri kuumia na dharau hii toka kwa marafiki na wafanyakazi wenzangu, niwatakie maisha mema. MWISHO Poleni wazazi wangu, marafiki zangu na wote tulio kuwa pamoja naomba taarifa wapewe wazazi wangu na familia yangu kutoka musoma na tarime namba zao 0752431811." mwisho wa waraka huo wa kusikitisha. Ungemshauri nini fredrick kama ungepata nafasi kabla ya kifo chake.



u15179075_138270363318863_6455862868763144313_n.jpg
Marehemu fredrick enzi za uhai wake
MANENO YA MWISHO YA FREDRICK KABLA YA KUJIUA


HATIMAE JANA CHINA WAADHIMISHA MWAKA MPYA

WACHINA WALIVYOSHEHEREKEA MWAKA MPYA WAO KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Jamhuri ya Watu wa China zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea hundi ya shilingi milioni 70 kutoka kwa  Balozi wa China nchini Mhe. Dk. Lu Youqing iliyotolewa na Taasisi pamoja na Jumuiya ya Wachina wanaoishi Tanzania kuchangia shule ya msingi ya Chato iliyopo mkoani Geita wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni wengine waalikwa pamoja na wasanii waliotumbuiza wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
 Sehemuya watu waliohudhuria sherehe za mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe. Dk. Lu Youqing wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam
                         

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania itaendelea kudumisha,kuimarisha na  kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na China kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande hizo MBILI.
 
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam katika sherehe ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina hapa nchini sherehe ambazo zimehudhuriwa na mamia ya raia wa China na Tanzania.
 
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa China imekuwa mshirika na mdau mkubwa wa maendeleo hapa nchini na hali hiyo inatokana na mahusiano mema na mazuri yaliyopo kati ya nchi hizi Mbili.

 
Makamu wa Rais amemhakikishia Balozi wa China hapa nchini Dkt Lu Youqing kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli itakuwa bega kwa bega na serikali ya China hasa katika uimarishaji wa sekta za biashara, utamaduni, elimu, afya  na masuala ya kijeshi kwa ajili ya maslahi na ustawi wa wananchi wa Tanzania na China.
 
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kujifunza mambo mengi kutoka China ili kuharakisha shughuli za maendeleo za wananchi kutokana na Taifa la China kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

 
Amehimiza ubadilishanaji wa wataalamu kati ya Tanzania na China katika sekta mbalimbali kama hatua ya kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi nchini.
 
Kwa Upande wake, Balozi wa China hapa nchini Dkt Lu Youqing amepongeza hatua zinachukuliwa na serikali ya Tanzania katika kupambana na rushwa na ufisadi.
 
Dkt  Lu Youqing amesema serikali ya China na raia wake wanafurahishwa na hatua hizo kwa sababu zinalenga kuondoa na kukomesha rushwa na ufisadi kwani tabia hizo zikiachwa ziendelee zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha utoaji wa huduma bora na za msingi kwa wananchi.

 
Akizungumzia mwaka mpya wa Kichina hapa nchini Balozi huyo amesema maadhimisho hayo ni muhimu kwa sababu raia Wachina na Tanzania wanajumuika pamoja katika kubadilisha mawazo na kutakiana heri na mafanikio kwa mwaka 2017.
 
Balozi huyo wa Tanzania hapa nchini Dkt  Lu Youqing pia amewashukuru wananchi wa Tanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mnazi Moja katika kusheherekea sikukuu ya Mwaka mpya wa Kichina sherehe ambazo inapambwa na michezo mbalimbali ikiwemo sarakasi na vikundi vya ngoma asili kutoka China na maonyesho.
Katika Maadhimisho hayo, Balozi wa China nchini Tanzania Dkt  Lu Youqing amemkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mfano wa hundi ya shilingi milioni 70 fedha ambazo zitatumika katika ujenzi kwenye shule ya msingi Chato iliyopo mkoani Geita.

SASA NYAMA YAANZA KUTENGEEZWA MAABARA.

Written by john jbp

Kutokana na ukuaji wa sayansi na teknolojia mambo kadha wa kadha yagundulika likiwemo hili la nyama. Fahamu hapa zaidi
DUNIA inabadilika kwa haraka kutokana na maendeleo katika sekta mbalimbali. Teknalojia nayo inakua kwa kasi huku ikitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya binadamu. Siku hizi Dunia inashuhudia uvumbuzi wa teknalojia za kisasa katika nyanja za kilimo, afya, nishati na nyingine nyingi.

Leo katika safu hii, nitajadili namna ambavyo wanasayansi walivyofanya jitihada za kutengeneza nyama katika maabara. Ndiyo, sasa si lazima kuhangaika kufuga na kupata usumbufu wa kutunza wanyama ili uweze kupata nyama.

Wote mtakubaliana na mimi kuwa, aina zote za vyakula vinavyotumiwa na binadamu inatokana na mimea na wanyama. Mamilioni ya wanyama huchinjwa kila siku duniani kwa ajili ya kupata kitoweo. 
Uchinjaji wa wanyama umekuwa mkubwa kuliko uzalishaji jambo ambalo limewafanya wanasayansi kufikiri namna ya kutengeneza kitoweo hiki muhimu pasipo kuhusisha kuchinja mnyama.

Rasilimali nyingi zimekuwa zikitumika kulisha wanyama, kuwachinja na kusafirisha, pia kumekuwapo upotevu mkubwa wa maji na nishati katika mzunguko mzima wa kupata kitoweo hiki. 
Ufugaji wa wanyama ambao hutupatia nyama unazalisha gesi ya methane ambayo inamchangio mkubwa katika mabadiliko ya tabianchi, wanasayansi wanataka kuondokana na haya yote kwa kutafuta mbinu mbadala ya kuzalisha nyama.

Kwa upande mwingine, wanyama hufungiwa ndani kwa maisha yao yote. Wanyama pia huchinjwa kikatili ili kuweza kupata nyama. Pamoja na haya yote, ni vigumu kufikiri maisha ya binadamu bila kula nyama. 
Utamaduni wa kula nyama ni mkongwe duniani na kwa vyovyote vile haitakuwa rahisi kuufuta. Kwa kutambua ukweli huu, wanasayansi wameaanza kutengeneza nyama maabara waliyoipa jina la nyama ya Vitro au Vitro meat kwa kimombo.

Nyama ya Vitro huzalishwa maabara. Kwa kawaida nyama hutengenezwa kutokana na kemikali ndogo inayojulikana kitaalamu atoms. Kama unaweza kutengeneza atoms kwa njia tofauti na ya kawaida, basi pia unaweza kutengeneza nyama. 
Ukipewa vipande viwili vya nyama kimoja kilichotokana na mnyama aliyechinjwa na nyingine aina ya Vitro ambayo hutengenezwa maabara ni vigumu kuelezea tofauti yake kutokana na kufanana kwa muonekano na hata ladha.

Maabara sasa inafanya kazi ya kutengeneza nyama ambayo ni sawa na nyama uliyozoea kununua buchani. Profesa wa Molecular Biology, katika Chuo Kikuu cha Stanford, alinukuliwa na gazeti la The Gurdian la Uingereza akisema inawezekana kuondokana na usumbufu wa kufuga na kuchinja wanyama kwa kuwa nyama sasa inaweza kutengenezwa maabara.

“Sina nia ya kutengeneza vyakula vipya kwa watu wasiokula nyama. Natengeneza chakula kwa ajili ya wanaokula nyama na ambao wana nia ya kula nyama. Hii itawasaidia kupata nyama bila shurba.

“Nyama ya Vitro haitokani na kiumbe hai hivyo haiwezi kufa na hii naletea tofauti kubwa katika upatikanaji wake. Kiuchumi, gharama za uzalishaji wake ni kubwa na hivyo kufanya uzalishaji mkubwa kuwa changamoto. 
Pia kutokana na ushawishi wa wafugaji wakubwa Marekani na sehemu nyingine duniani, inawezekana kuwa na vikwazo vya kisheria,” anasema Profesa huyo.

Gharama kubwa za uzalishaji wa nyama ya Vitro inaweza kuwa ndiyo kikwazo kikubwa katika uzalishaji wake. Hata hivyo, ugunduzi zaidi kwenye teknalojia ya uzalishaji wake itaweza kupunguza gharama. 
Kampuni kubwa ikiwamo New Harvest na Modern Meadow zinafanya kazi kuhakikisha kuwa nyama hii inazalishwa kwa wingi na kuwafikia walaji wengi.

SAMATTA AIPA GENK POINT 3 ZA MUHIMU.

Written by john jbp

SAMATTA AWAPA USHINDI GENK BAADA YA KUFUNGA GOLI PEKEE LA USHINDI.
Mbwana Samatta ameifungia KRC Genk bao pekee wakati ikiitwanga Eupen katika Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Genk imeshinda 1-0 baada ya Samatta kufunga bao hilo katika dakika ya 82 akiunganisha basi safi ya Ruslan Malinovysky.

Samatta ambaye amecheza kwa dakika zote 90, alionyesha uwezo mkubwa ikiwa ni pamoja na kuwapa wakati mgumu mabeki wa Eupen.

Kama si juhudi za kipa wa Eupen Hendrik van Crombrugge, Samatta ambaye ni nahodha wa Taifa Stars angeweza kufunga mabao mengine.


Kwa ushindi huo Genk imesogea hadi katika nafasi ya nane ikiwa na pointi 31, huku Club Brugge ikiendelea kuwa kinara wa Ligi Kuu Ubelgiji ikiwa na pointi 43.

   

HATIMAE YAHYA JAMMEH AONDOKA NCHINI GAMBIA.

Written by John jbp
JAMMEH AONDOKA GAMBIA RASMI
Aliyekuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh ameondoka nchini humo baada ya mvutano wa muda kufuatia kushindwa katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Disemba Mosi mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ECOWAS, kiongozi huyo aliyeiongoza Gambia kwa miaka 22 alipanda ndege kuelekea nchini Guinea ambapo akifika atasafiri kwenda nchini Equatorial Guinea atakapoishi uhamishoni.

Yahya Jammeh is to go into exile in Equatorial Guinea

Jammeh alishindwa na kiongozi wa upinzani, Adama Barrow ambaye amekuwa akiishi nchini Senegal na kueleza kuwa atarudi Gambia usalama ukiimarika.

Barrow aliyeapishwa katika Ubalozi wa Gambia nchini Senegal, alisema kuwa akiingia madarakani ataunda tume kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na Yahya Jammeh katika kipindi cha miaka 22 ya utawala wake.

Rais wa ECOWAS, Marcel de Souza pia ameeleza kuwa wanajeshi waliokuwa wametumwa kutoka nchi wanachama kwenda kumuondoa Jammeh madarakani sasa wataondolewa japo wachache watabaki kuendelea kuimarisha usalama.

Wananchi wa Gambia wamekuwa na hisia tofauti kuhusu kuondoka kwa Jammeh ambapo wanaoaminika kuwa ni wafuasi wake walisikitika kwa majonzi alipokuwa akiwaaga katika uwanja wa ndege huku wengine wakishangilia kuamini kuwa ni mwisho wa utawala wa kidikteta uliokuwa hauheshimu haki za binadamu.

Kitu alichoahidiwa Jammeh kuweza kuachia madaraka baada ya kukutana na baadhi ya viongozi wa mataifa mengine bado hakijafahamika.

Yahya Jammeh anakuwa Rais wa kwanza wa Gambia kuondoka madarakani kwa amani tangu walipopata uhuru mwaka 1965.

Friday, 13 January 2017

AZAM FC YAFANIKIWA KUTWAA KOMBE LA MAPINDUZI 2016

Timu ya wanalambalamba wa chamanzi almaarufu kama AZAM FC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mapinduzi 2016 ikiwa mara yao ya 3 tangu waingie kushiriki kombe hilo.Azam wameifunga simba goli 1 kipindi cha kwanza kupitia kiungo hodari HIMID MAO (mkami).

     

             
   
   

AJIRA MPYA KWA WALIMU WA DIPLOMA NA DEGREE

Majina ya ajira mpya kwa walimu wa ngazi ya stashaada na shahada ya sayansi.
    Bonyeza link kuangalia
https://drive.google.com/open?id=0B_s3POlqJhTUNEk3Z2dTRGdXTmM
   
   https://drive.google.com/open?id=0B_s3POlqJhTULXZaT1lfM0JzMFk


Thursday, 22 December 2016

KAZI NZURI ZAIDI KUWAHI KUTOKEA DUNIANI.

               Habari ndugu msomaji, niko tayari kukujuza zaidi mambo unayoyafahamu na yale usiyo yafahamu. Leo katika jua zaidi nina hili, Roald Dahl (1916-1990) ndiye mwanaume anaye tajwa kuwahi kuwa na kazi nzuri zaidi duniani. Hiyu alikuwa mwingereza aliye ajiriwa na serikali ya uingereza kama mpelelezi (spy) lakini kazi yake ilienda mbali zaidi alipotakiwa kuwatongoza wanawake maarufu na wenye pesa kutoka marekani ili aweze kulala nao kwa nia moja tu ya Kuchunguza habari muhimu na za ndani ya serikali ya marekani. Serikali ya uingereza iliamini kuwa ni rahisi kuifahamu zaidi serikali ya marekani kupitia wanawake mashughuli na wenye pesa kwa kuwa wana ukaribu na viongozi wa kiserikali.
Image result for roald dahl
Roald Dahl(mwandishi wa stori fupi na riwaya kutoka marekani pia mpelelezi wa chinichini)
Kesho pia ni siku tukutane hapahapa kwenye blog yako pendwa ya johnjbp.blogspot.com tupate kujuzana mambo mengi zaidi. Jua zaidi




by, johnjbp.